Nukuu Papo Hapo na Arifa kuhusu Sauti
-
4.1
: hakiki za hesabu -
4.3.366152410 Version
Zaidi Matoleo
Arifa za matukio yenye sauti na manukuu ya mazungumzo yako kwa wakati halisi
Programu ya Nukuu Papo Hapo ina jina jipya — Nukuu Papo Hapo na Arifa kuhusu Sauti. Ni programu inayozifanya sauti za mazingira na mazungumzo ya kila siku kupatikana kwa urahisi na watu wenye tatizo la kusikia na viziwi, kwa kutumia tu simu yako ya Android.
Kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya Google ya utambuzi wa matamshi na sauti kiotomatiki, Nukuu Papo Hapo na Arifa kuhusu Sauti inakupa manukuu ya mazungumzo yako kwa wakati halisi bila malipo na kutuma arifa kulingana na sauti za mazingira ya nyumbani. Arifa hukujulisha kuhusu hali muhimu nyumbani, kama vile kengele ya moto au kengele ya mlango inapolia, ili uweze kuchukua hatua kwa haraka.
Kwenye simu nyingi, unaweza kufikia Nukuu Papo Hapo na Arifa kuhusu Sauti moja kwa moja ukitumia hatua hizi:
1. Fungua programu ya Mipangilio ya kifaa chako.
2. Gusa Ufikivu, kisha uguse Nukuu Papo Hapo au Arifa kuhusu Sauti, kulingana na programu ambayo ungependa kufungua.
3. Gusa Tumia huduma, kisha ukubali ruhusa.
4. Tumia Ishara au kitufe cha zana za ufikivu ili ufungue programu ya Nukuu Papo Hapo au Arifa kuhusu Sauti.
[Mpya] Arifa kuhusu Sauti:
• Arifiwa kuhusu hali hatari na hali za binafsi zinazoweza kutokea kulingana na sauti zinazofanyika nyumbani (kwa mfano kengele ya moshi, king'ora, sauti za watoto).
•Pokea arifa kupitia mweko au mtetemo kwenye kifaa chako cha mkononi au kifaa kinachovaliwa.
• Mwonekano wa rekodi ya maeneo uliyotembelea hukuruhusu kurejelea historia (kwa sasa inaweza tu kutumika kwa saa 12) ili uone kilichofanyika karibu nawe.
Unukuzi kwa muda halisi:
• Hunukuu katika muda halisi. Maandishi huonekana kwenye simu yako maneno yanapotamkwa.
• Hurekodi kwa usahihi tofauti za jinsi maneno yanavyotumika katika muktadha.
• Chagua kutoka zaidi ya lugha na lahaja 80, na ubadilishe kwa haraka kati ya lugha mbili.
• Weka maneno maalum unayotumia mara kwa mara, kama vile majina au bidhaa za nyumbani.
• Weka simu yako katika hali ya kutetema mtu anapotamka jina lako.
• Andika majibu katika mazungumzo yako. Fungua kibodi ya simu yako na uandike maneno yako ili uendeleze mazungumzo. Bado manukuu yanaonekana unapoandika.
• Angalia kiwango cha sauti ya mzungumzaji ikilinganishwa na kiwango cha sauti katika mazingira yako. Unaweza kutumia kiashirio hiki cha sauti kurekebisha sauti ukizungumza.
• Tumia maikrofoni za nje zinazopatikana kwenye vifaa vya sauti vinavyotumia waya, vifaa vya sauti vya Bluetooth na maikrofoni za USB kwa upokeaji mzuri wa sauti.
Kurejelea unukuzi tena:
• Chagua kuhifadhi manukuu kwa siku tatu. Manukuu yaliyohifadhiwa yatasalia kwenye kifaa chako kwa siku tatu, ili uweze kuyanakili na kuyabandika kwingineko. (Kwa chaguomsingi, manukuu hayahifadhiwi.)
• Tafuta katika manukuu yaliyohifadhiwa.
• Gusa na ushikilie maandishi katika manukuu ili unakili na kubandika.
Mahitaji:
• Android 5.0 (Lollipop) na matoleo mapya zaidi.
Nukuu Papo Hapo na Arifa kuhusu Sauti ilitengenezwa kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Gallaudet, chuo kikuu kinachosifika cha viziwi na walio na matatizo ya kusikia nchini Marekani.
Jiunge na Jumuiya ya Ufikivu kwenye Google ili utoe maoni na upokee taarifa za bidhaa. Ili upate usaidizi wa kutumia Nukuu Papo Hapo na Arifa kuhusu Sauti, wasiliana na timu ya Usaidizi kwa Walemavu.
Ilani ya Ruhusa
Maikrofoni:Programu ya Nukuu Papo Hapo inahitaji kufikia maikrofoni ili kunukuu matamshi yaliyo karibu nawe. Haihifadhi sauti baada ya kuchakata manukuu. Programu ya Arifa kuhusu Sauti inahitaji kufikia maikrofoni ili iweze kusikiliza sauti zinazofanyika karibu nawe. Haihifadhi sauti pia baada ya kumaliza kuchakata.