Kikuza Sauti
-
4.1
: hakiki za hesabu -
3.0.344165751 Version
Zaidi Matoleo
Chuja, ongeza na ukuze sauti zilizo karibu nawe na kwenye kifaa chako.
Kikuza Sauti huboresha sauti kutoka maikrofoni ya kifaa chako cha Android kwa kutumia vipokea sauti vinavyobanwa kichwani ili kuboresha hali ya usikilizaji. Tumia Kikuza Sauti ili uchuje, uongeze na ukuze sauti karibu nawe na kwenye kifaa chako. Kikuza Sauti huongeza sauti muhimu, kama vile mazungumzo, bila kuongeza kiwango cha sauti ya kelele zinazosumbua. Kwa kutumia vitelezi viwili rahisi, unaweza kuweka mapendeleo ya uboreshaji wa sauti na kupunguza kelele za chinichini kwa haraka.
Inapatikana kwa vifaa vinavyotumia toleo la Android la 6.0 na matoleo mapya. lli uanze kutumia Kikuza Sauti, unganisha vipokea sauti vyako vinavyobanwa kichwani (vinavyotumia waya au Bluetooth) kisha uende kwenye Mipangilio > Ufikivu > Kikuza Sauti.
Vipengele
• Imarisha sauti muhimu na upunguze kelele zinazosumbua na zisizohitajika karibu nawe na kwenye kifaa chako.
• Silikiza mazungumzo au utumie vipokea sauti vinavyobanwa kichwani vya Bluetooth ili vikusaidie kusikia mambo kama vile vipindi vya TV na mihadhara. (Vipokea sauti vinavyobanwa kichwani vya Bluetooth vinaweza kupokea sauti kwa kuchelewa.)
• Chuja, ongeza na ukuze video na sauti inayocheza kwenye simu. (Inapatikana kwenye simu za Pixel zinazotumia toleo la Android 10, sasisho la Desemba 2019 au sasisho jipya zaidi la mfumo.)
• Weka mapendeleo ya hali yako ya usikilizaji kwa kubadilisha mipangilio ya sauti au maikrofoni ukitumia kiolesura rahisi cha kurekebisha sauti.
• Angalia kinachoendelea karibu nawe ukitumia madoido ya sauti.
Baada ya kuwekea Kikuza Sauti mipangilio unayopenda, unaweza kukiwasha na kukizima ukitumia Kitufe cha Zana za Ufikivu.
Ilani ya Ruhusa
• Simu: Hali ya simu itaruhusu Kikuza Sauti kisimame wakati kuna simu unayopiga au inayoingia.
• Maikrofoni: Ufikiaji wa maikrofoni utaruhusu Kikuza Sauti kichakate sauti kwa ajili ya kukuza na kuchuja. Hakuna data inayokusanywa au kuhifadhiwa.