Toleo la haraka la Messenger linalofanya kazi kwenye hali zote za mtandao
Programu ya utumaji ujumbe iliyo na kasi na inayotumia data kidogo ili kuwafikia watu maishani mwako. Messenger Lite:
- Husakinisha haraka. Unaweza kupakua ukiwa na chini ya MB 10!
- Huhifadhi data. Inapakia haraka, huendeshwa kwa ufanisi na hutumia data kiasi ya kifaa cha mkononi.
- Hufanya kazi kila mahali. Fikia watu unapokuwa katika eneo lililo na muunganisho wa polepole au usio dhabiti wa intaneti.
Ukiwa na Messenger Lite, unaweza:
- Kuwasiliana na kila mtu kwenye, Messenger, Facebook au Facebook Lite.
- Angalia wakati watu wapo mtandaoni na wanapopatikana ili kupiga gumzo.
- Watumie watu ujumbe moja kwa moja au kwenye vikundi ili kuwasiliana au kuunda mipango.
- Tuma picha, viungo, au jieleze kwa vibandiko.
- Piga simu za moja kwa moja au simu za video bila malipo kupitia Wi-Fi (vinginevyo gharama wastani za data zinatekelezwa). Zungumza jinsi unavyotaka, hata na watu katika nchi zingine!