Daydream
-
3.4
: hakiki za hesabu -
1.23.190812026 Version
Zaidi Matoleo
Furahia Uhalisia Pepe bora kwenye simu inayoweza kutumia Daydream.
Kipengele cha Daydream kinaleta uhalisia pepe (VR) wa ubora wa juu katika simu zinazoweza kutumia kifaa hicho cha kutazama. Ukiwa na programu ya Daydream, unaweza kufungua maonyesho unayoyapenda ya uhalisia pepe na upitie mkusanyiko unaozidi kuongezeka wa programu na michezo. Gundua sehemu mpya za ulimwengu, jitulize katika sinema yako mwenyewe ya uhalisia pepe na ucheze michezo ya kusisimua inayokuweka katika mstari wa mbele wa matukio. Zaidi ya hayo, programu itapatia maudhui yaliyoangaziwa kipaumbele ili uwe na mapya ya kutazama ukivaa kifaa chako cha kutazama uhalisia pepe.
Vipengele:
• Weka mipangilio ya kifaa cha kutazama na kidhibiti kinachooana na Daydream
• Pitia na uweke programu popote ulipo au katika uhalisia pepe
• Fungua maonyesho ya Daydream unayoyapenda
Programu ya Daydream inahitaji kifaa cha kutazama uhalisia pepe kinachooana kama vile Daydream View na simu inayoweza kutumia kipengele cha Daydream kama vile Pixel. Pata maelezo zaidi katika http://g.co/daydream.
Kwa kutumia programu hii unakubali kuwa chini ya Sheria na Masharti yetu ya Google (Google ToS, http://www.google.com/accounts/TOS), Sera ya Jumla ya Faragha ya Google (http://www.google.com/intl/en/policies/privacy/), na masharti ya ziada yaliyo hapo chini. Programu hii ni Huduma kama inavyofafanuliwa katika Sheria na Masharti ya Google na matumzi yako ya programu hii yako chini ya masharti yanayohusu programu katika Huduma zetu.
Kabla ya kutumia programu ya Daydream, hakikisha kwamba watumiaji wote wamepitia Maelezo ya Afya na Usalama katika Kipengele cha Daydream yanayopatikana katika g.co/daydream/SafetyWarrantyReq.