Microsoft Kaizala
-
4.6
: hakiki za hesabu -
1.1.2926.5711 Version
Zaidi Matoleo
Kazi na gumzo la timu
Microsoft Kaizala ni programu mpya ya kifaa cha mkononi inayorahisisha kuwasiliana na kufanya kazi kwenye uga. Ukiwa na Kaizala, unaweza kufikia zana unazohitaji kusasishwa na kutekeleza majukumu kwa ufanisi. Kaizala hurahisisha kupata matangazo kutoka kwenye ofisi kuu, kutuma majibu kupitia kura au uchunguzi, au kupiga gumzo tu na wengine 1:1 au kwenye vikundi. Vikundi vya umma hukuwezesha kutuma majibu au kuripoti masuala kwa mashirika unayotaka kuungana nayo. Jibu kazi kwa midonoo michache tu na uendelee kufanya kazi yako kwa kupanga kazi ulizopangiwa.
Kipengele cha kipekee cha uhamasisho wa eneo la Kaizala hurahisisha kuomba eneo kutoka kwa wengine, kutuma eneo lako lililotambulishwa la kijiografia kwa mdonoo mmoja, au hata kupiga na kutuma picha huku eneo likiwa limetambulishwa kiotomatiki. Ni rahisi kuona mahali ambapo kila mtu anafaa kuratibu kazi kwa ufanisi.
Dhibiti siku yako bila tatizo ukitumia “Vitendo” vya Kaizala, vinayokuwezesha kufanikisha matukio ya kawaida ya kazi unapotumia kiolesura rahisi cha kupiga gumzo katika njia iliyopangwa. Vitendo vya Kaizala vinavyopatikana nje ya kikasha vinajumuisha: Matangazo - kufanya matangazo muhimu au kushiriki visasisho, Kazi - kuwapangia watu kazi na kufuatilia hali ya ukamilisho, Tukutane - kuwaalika watu kwenye mikutano na kuthibitisha hali yao ya upatikanaji, Eneo la Moja kwa Moja - kuomba eneo la moja kwa moja na uwasaidie watu wapate njia, Picha kwa Eneo - kushiriki picha pamoja na eneo lako la sasa, Kura ya Maoni ya Haraka - kuuliza swali na kupata maoni ya watu, Omba Eneo - kuwaomba watu washiriki eneo lao, Shiriki Eneo - kushiriki eneo lako na wengine, Wasilisha Bili - kuwasilisha bili na gharama zako, Uchunguzi - kuuliza msururu wa maswali na upate maoni ya watu, na Orodha angalizi - kuunda orodha za mambo ya kufanya na kunasa hali ya kila mtu.
Ni programu moja kwa mawasiliano ya kikundi na usimamiaji wa kazi. Ikague leo!
Tunathamini majibu yako. Tafadhali shiriki mawazo na majibu yako katika https://aka.ms/kaizalafeedback, jiunge kwenye mawasiliano katika https://aka.ms/discuss, au tuandike katika [email protected]
Kwa maelezo zaidi juu ya upatikanaji katika eneo lako tafadhali tembelea https://aka.ms/kaizala_availability
Kagua sheria na masharti: https://aka.ms/kaizala-eula
Kumbuka: Programu hii inaweza kutumia eneo lako hata wakati haijafunguliwa, inayoweza kusababisha kupunguza maisha ya betri ya kifaa.