Google Keep - Madokezo na Orodha
-
4.3
: hakiki za hesabu -
5.21.281.07.40 Version
Zaidi Matoleo
Google Keep
Nakili kwa haraka mawazo yako na ukumbushwe baadaye kwa wakati au mahali panapofaa. Tamka kumbukumbu popote ulipo na itaandikwa kiotomatiki. Piga picha bango, stakabadhi au hati na uipange kwa urahisi au uipate baadaye katika utafutaji. Google Keep hufanya iwe rahisi kunakili wazo au orodha yako, na uishiriki na marafiki na familia.
Nakili mawazo yako
• Ongeza madokezo, orodha na picha kwenye Google Keep. Je, huna wakati? Rekodi kumbukumbu ya kutamka na Google Keep itaiandika ili uipate baadaye.
Shiriki mawazo na marafiki na familia
• Panga sherehe ya kushtukizia kwa urahisi kwa kushiriki madokozo yako ya Google Keep na watu wengine, na ushirikiane nao katika wakati halisi.
Pata kwa haraka unachohitaji
• Weka rangi na lebo kwenye madokezo ya msimbo ili upange kwa haraka na uendelee na maisha yako. Kama unahitaji chochote ulichohifadhi, utakipata kwa urahisi kupitia utafutaji.
Hupatikana kila wakati
• Google Keep hutumika kwenye simu yako, kompyuta kibao, kompyuta ya kawaida na vifaa vya kuvaliwa vya Android. Kila kitu unachoongeza husawazishwa kote kwenye vifaa vyako, kwa hivyo huwezi kusahau chochote.
Dokezo linalofaa kwa wakati unaofaa
• Unahitaji ukumbushwe kununua bidhaa yoyote? Weka kikumbusho kinachotegemea mahali ili upate orodha ya bidhaa wakati unapofika dukani.
Hupatikana kila mahali
• Jaribu Google Keep kwenye wavuti ukitumia http://keep.google.com na uipate kwenye Duka la Wavuti la Chrome ukitumia http://g.co/keepinchrome.
Taarifa ya Ruhusa
Kamera: Hii inatumiwa kuambatisha picha kwenye madokezo ya Google Keep.
Anwani: Hii inatumiwa kushiriki madokezo na watu unaowasiliana nao.
Maikrofoni: Hii inatumiwa kuambatisha madokezo ya sauti.
Mahali: Hii anatumiwa kuweka na kuanzisha vikumbusho vinavyozingatia mahali.
Hifadhi: Hii inatumiwa kuongeza viambatisho kutoka kwenye hifadhi katika madokezo.