Find My Kids: Fuatilizi ya saa ya GPS na rununu
-
4.6
: hakiki za hesabu -
2.3.29 Version
Zaidi Matoleo
Chaguo la Mhariri! Fuatilizi ya GPS. Pata wana kwenye ramani. Sauti ya karibu
“Find My Kids” ni programu ya familia inayofuatilia mfumo wa mwongozo kuhakikisha usalama wa watoto na tawala ya mzazi. Unaweza kuunganisha mfumo wa mwongozo au kuweka programu hii kwenye rununu ya mwanao ili ujue eneo lake.
"Find My Kids" ni programu fuatilizi inayotumiwa na wazazi na kuondoa wasiwasi watoto wakiwa mbali na mzazi na hawasikii rununu ikilia.
✔ Kifuatilizi cha GPS – Fuatilia aliko mwanao kwenye ramani na historia ya mwenendo wa siku kuhakikisha mtoto haendi maeneo hatari.
✔ Sauti iliyo karibu – Sikiliza kinachoendelea kwenye mazingira ya mwanao kuhakikisha yuko salama na anashirikiana na watu wazuri.
✔ Kionyo cha Kamsa – Tuma kionyo kwenye rununu ya mwanao anapoiwacha mkobani au anapoiweka kimya na kukosa kusikia ikilia.
✔ Udhibiti wa Programu za Rununu – Vumbua programu zitumiwazo shuleni na ikiwa walicheza darasani badala ya kusoma.
✔ Udhibiti wa Usalama – Angalia mtoto ikiwa mtoto amefika shuleni kwa wakati unaofaa – pata taarifa akifika shuleni, akirudi nyumbani na maeneo mengine uliyoongeza mwenyewe.
✔ Udhibiti wa Betri – Fuatilia kiwango cha chaji, kumbusha mtoto kutia chaji, programu itatuma ujumbe betri ikiisha nguvu.
✔ Gumzo za Familia – Tumia stika za ucheshi kupiga gumzo na mwanao.
Programu ya Tawala ya Mzazi
Programu ya kufuatilia ya “Find My Kids” imekusudiwa kuhakikisha usalama wa familia na tawala ya wazazi tu. Haiwezi kuwekwa kwenye rununu kisiri, matumizi yanaruhusiwa tu kwa idhini ya mtoto. Habari binafsi huhifadhiwa kulingana na sheria na sera za GDPR.
Tunajali faragha na usalama wa taarifa zako. Kwa hivyo programu zetu zinawiana na taratibu za COPPA, sheria inayolinda watoto mtandaoni, inayodhibitishwa na cheti cha COPPA kidSAFE Seal Program.
Ikiwa mwanao ana rununu mahiri:
Weka programu ya Pingo! kwenye rununu yake – kifuatilio cha mfumo wa mwongozo cha mtoto. Kwenye programu ya Pingo! ataweza kukutumia jumbe fupi, iwapo kuna hatari, atabonyeza kidude cha dharura. Anapobonyeza kidude cha SOS, utapata kionyo cha kamsa kwenye simu yako.
Ikiwa mwanao ana saa ya mfumo wa mwongozo:
Unganisha na programu inayoaminika ya “Find My Kids” yenye ujabinishaji wa ndani na msaada wa kiufundi. Programu hii inatumika kwenye vifaa hivi: Smart Baby Watch, Smart Age Watch, Smart Pet Tracker, Smart Tracker, Wonlex, Titan Watch na vifaa sawa.
Ukitarajia kununua saa mahiri inayotumia mfumo wa mwongozo, tunapendekeza aina ya Smart Baby Watch kama vile Q8, W10, Q360, DS18, G10, na 18. Chaguo zingine ni W8, Q50, na Q80. Ukipendezwa na kifaa cha hali ya juu zaidi, tafuta Tiroki Q8, OJOY A1 au saa za Amoto.
Programu ya “Find My Kids” hufanyaje kazi:
1) Weka programu ya “Find My Kids” kwenye rununu yako;
2) Chagua kifaa cha kuunganisha: rununu ya mtoto au saa ya mfumo wa mwongozo;
3) Weka programu ya Pingo! kwenye simu ya mtoto au weka nambari ya kadiwia ya saa ya mfumo wa mwongozo.
Ukiwa na matatizo ya kiufundi, wasiliana na wasaidizi wetu kupitia kituo cha mazungumzo au tuma barua pepe kwa [email protected].
Unaweza kutumia vipengele vyote bila malipo wakati wa kipindi cha majaribio baada ya kuunganisha na kifaa cha mtoto. Baada ya kipindi hiki, bado utaweza kuona eneo la mtoto wako kwenye mtandao. Unahitaji kuwa na sajili baadaye ili kutumia vipengele vyote.
Programu ya "Find My Kids" huomba ruhusa zifuatazo:
– ufikivu wa kamera – kuweka picha ya wasifu ya mtoto;
– ufikivu wa waasiliani – kujaza kitabu cha simu kwenye simu ya mfumo wa mwongozo;
– ufikivu wa kinasa sauti – kutuma jumbe za sauti katika kituo cha maongezi.